Nafasi Ya Matangazo

July 01, 2016

SHIRIKA la ndege la kitanzania Precision Air linatarajia kurudisha safari zake za ndege kati ya DAR ES SALAAM na HAHAYA nchini Comoro ifikapo Agosti 16, 2016. 

Hapo Awali Precision Air ilisitisha safari zake za kwenda HAHAYA mwaka 2014 katika utekelezaji wa mpango wake wa miaka 5 mitano uliouhusisha uimarishaji wa mtandao wa safari kwa kuzingatia tija.

Taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa biashara Precision Air, Robert Owusu imesema kwamba baada ya Precision Air kuimarisha idadi ya ndege zake, imeona ni wakati muafaka kurudisha safari za HAHAYA.

“ Tunafahamu kuna mahitaji makubwa ya safari kati ya Dar es Salaam na Hahaya, na baada ya kujitathimini na kujiridhisha na uwezo wetu, tumethibitisha ya kuwa hatuna budi kurudisha safari za Hahaya sasa. Idadi ya ndege zetu ikoimara zaidi na hii inaweza thibitishwa na kuimarika kwa safari zetu zinazofanyika kwa wakati ambapo kwa miezi kadhaa sasa asilimia 90 ya safari zetu zilifanyika kwa wakati uliopangwa,” alisema Owusu.

Owusu alisema kwamba safari za Precision Air kati ya Dar es Salaam na Hahaya zitaimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Comoro na kwamba Precision Air itafanya safari mara tatu kwa wiki kila siku ya Jumanne, Alhamisi, na Jumamosi.

“Kuna wafanyabiashara wengi wanoa fanya biashara kati ya Dar es Salaam na Hahaya na tunauhakika safari zetu zitawafaa sana kwa  kuwaongezea tija katika biashara zao. Tiketi zetu zinajumuisha kilo 23 za mizigo bure hivyo basi wafanyabiashara wataweza kusafirisha mizigo yao kwa urahisi watakapo safari nasi.” 

Safari za Precision Air zinatarajiwa kuwawezesha watalii pamoja na wanataaluma mbalimbali kufanya safari zao kati ya Comoro na nchi za Ulaya,marekani na Uarabuni. 

Hahaya itakua safari yake ya pili ya kikanda ukiacha ile ya Nairobi. Precision Air ina safari kwenda maeneo 11 ndani ya nchi na ikiruka kutokea Dar es Salaam inasafiri kwenda Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba, Musoma, Tabora, Kigoma, Mtwara, Zanzibar na Pemba. 
Posted by MROKI On Friday, July 01, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo