Nafasi Ya Matangazo

July 25, 2016

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati), akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya tiketi ya ndege ya kwenda Dubai kwa mshindi wa kampeni ya ‘Shinda na TemboCard’, Juliana Utamwa (kushoto) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaama, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Dorisia Nanage ambaye ni ndugu yake atakayeambatana naye.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Dubai mshindi wa kampeni ya ‘Shinda na TemboCard’, Juliana Utamwa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaa.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Dubai, Dorisia Nanage ambaye ataambatana na mshindi wa kwanza, Juliana Utamwa.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakishuhudia tukio hilo.
 Mshindi wa Kampeni ya 'Shinda na TemboCard', Juliana Utamwa akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tiketi ya ndege ya kwenda Dubai na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), katika hafla ya makabidhiano ya zawadi kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Maofisa wa benki ya CRDB wakishuhudia tukio la kukabidhi tiketi kwa washindi wa Kampeni ya 'Shinda na TemboCard'
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Posted by MROKI On Monday, July 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo