Nafasi Ya Matangazo

June 30, 2016

Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga. na kushoto ni Kamishina wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Peter Dickson.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga.(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. katikati ni Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto  na kushoto ni Kamishina wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Peter Dickson.
Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kupandisha watu 50 katika kilele cha mlima Kilimanjaro na waendesha baiskeli 50 kuuzunguka mlima huo kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Tenga Tenga.
*************
MGODI wa Dhahabu wa Geita, Ukishirikiana na Tume ya kudhibiti Ukimwi, kwa mwaka wa 15 tangu kuanzishwa kwake, unatarajia kupandisha watu katika kilele cha Mlima Kilimanjaro watu 50 na kundi lingine lenye watu 50 watauzunguka mlima kwa baiskeli ili kuchangisha fedha kwaajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi hapa Tanzania.

Tukio hili limnatarajiwa kufanyika Julai 16 hadi 22 mwaka huu na watu kutoka mataifa mbalimbali watashiriki katika tukio hilo la kihistoria.

“Huu ni mwaka wa 15 tangu kuzishwa kwa Kili Challenge kwa hivyo tumedhamiria kufanya tukio hili kuwa tukio la kihistoria,” alisema Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga.

Tukio hili ambalo hufanyika kila mwakalilizinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais (Muungano na Mazigira) Januari Makamba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Kili Challenge katika mwaka huu itakuwa na kundi kubwa la watu kutoka nchi mbalimbali lakini wengi wakiwa watanzania kutoka katika sekta binafsi, serikalini, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na watu mbalimbali waliojitolea ili kutunisha mfuko huu wa Kili Challenge. Balozi wa Kili Challenge, Mrisho Mpoto ndie ataambatana na kundi hili hadi kileleni.

Balozi wa Kili Challenge, Mrisho Mpoto alisistiza watanzania kutambua kwamba mapambano dhidi ya Ukimwi ni yetu sisi watanzania na tunapaswa kuamua kuunga mkono jitihada za serikali kwa ajili ya kupambana ili kufikia sifuri 3.

“Mimi kama balozi wa Kili Challenge, naamini kwamba jitihada zinazfanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na watanzania wote na wadau wenyemachungu na nchi hii. Hebu tuungane kwa pamoja kila mmoja wetu katika sehemu yake eidha kwa kuchangia au kumuelimisha mwenzake ili mapambano haya yalete mabadiliko,”alisema Mpoto.

Mwakilishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (tacaids), Dickson Peter alisema Fedha zinazopatikana katika mfuko huu zinapelekwa kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kujenfa vituo vya ushauri nasaha na upimaji wa ukimwi ambapo baadhi yao ni vile vilivyopo mkoani Tanga pale Segera, Manyoni na Geita. Kituo cha watoto  yatima Moyo wa Huruma na Asasi nyingine zaidi ya 30 zimenufaika na mfuko huu.

Tenga alisema GGM inapenda kutambua michango ya wadau wengine wanaochangia mfuko huu kama vile, ACACIA, Prime fuel, Airtel, Capital Drilling (T)Ltd na wengineo.
Posted by MROKI On Thursday, June 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo