Nafasi Ya Matangazo

June 05, 2016

 Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wakishiriki kusafisha mazingira ya eneo la Ilala kota jijini Dar es Salaam,jana katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wakishiriki kusafisha mazingira ya eneo la Ilala kota jijini Dar es Salaam,jana katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani
 Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wakikabidhi baadhi ya vifaa vya kufanyia usafi kwa viongozi wa serikali ya mtaa wa eneo la Ilala jijini Dar es Salaam
KAMPUNI ya  TBL Group wameshiriki kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa vitendo ambapo wameshiriki katika zoezi la kusafisha mazingira katika eneo la Ilala Kota  kwa kushirikiana na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo pia kampuni imetoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 6 kwenye kata hiyo.

wafanyakazi wa viwanda vingine vilivyopo chini ya kampuni pia wameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya viwanda vyao na maeneo  ya jirani kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Akiongea juu ya maadhimisho hayo Meneja wa kiwanda  cha TBL cha Ilala,Calvin Martin amesema kuwa   wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group  popote walipo wameshiriki kuadhimisha siku hii  kwa kuwa mazingira ni moja ya mtazamo  wa kampuni ambapo imelenga kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira.

“ Moja ya malengo ya kampuni ni kujenga  dunia imara na dunia iliyo safi ambayo yamelenga kupata raslimali ya pamoja ya maji ya kutosha ambayo inatumika kwa kiasi kikubwa katika biashara ya kampuni.Katika kutekelea lengo hili kampuni kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele  kulinda na kutunza vyanzo vya maji na kuhakikisha maji yanayopatikana yananufaisha jamii ya wananchi inayowazunguka”alisema Calvin.

Calvin aliongeza kusema kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani mwaka huu isemao  “Tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu”.inakwenda sambamba na malengo ya  kampuni ya TBL Group ambayo pia ina mkakati wa kuelimisha jamii kutunza vyanzo vya maji na kusaidia kuendeleza miradi ya maji nchini.

Alisema katika kutekeleza utunzaji wa mazingira kwa vitendo TBL Group imeanza kufanya uzalishaji wa kutumia  pumba za mpunga katika kiwanda chake cha Mwanza na inafanya mkakati kuhakikisha inafanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira katika viwanda vyake vyote,

“Kampuni mama ya SABMiller imejiwekea malengo hadi kufikia mwaka 2020 kuhakikisha inafanya uzalishaji kwenye viwanda vyake usio na athari za mazingira hususani uchafuzi wa hali ya hewa au kufanya uharibifu wa mazingira wenye athari kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo vilipo viwanda vyake kwa asilimia 50% na tayari hadi kufikia sasa imepunguza uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na uzalishaji kwa asilimia 35% tangia kuanza kwa mkakati huu mnamo mwaka 2008”.Alisema.
Posted by MROKI On Sunday, June 05, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo