Nafasi Ya Matangazo

June 01, 2016


Asalaam Alaykum Warhmatu llahi Wabarakatu.

Ikiwa Zimebaki Siku Chache kuingia au kutufikia Mgeni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ... "Tunamuomba M/Mungu atubariki katika masiku yaliyo baki ya Mwezi wa Shaaban na atufikishe Mwezi Mtukufu wa Ramadhan" Allahumma Ameen . 

Katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani tunawaletea Program ya kheri ifuatayo. 

MFUTURISHE NDUGU YAKO MUISLAM  KWA KUFUATA SUNNA YA MTUME MUHAMMAD (REHMA ZA M/MUNGU ZIMSHUKIE JUU YAKE NA AMANI) Kwa KOKWA YA TENDE AU MAJI.

Mahitajio.

1.Carton za Maji kwa Idadi uwezayo kwani Matarajio ya Program hii ni Mwanzo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Mpaka Mwisho wa Mwezi wa Mfungo. (MAJI tunayo hitaji ni Robo lita au Nusu lita ) 

2.JUICE ... (Ndogo Maarufu zinaitwa za kijoti) SADAKA KWA AJILI YA WATOTO WADOGO (ZIADA KATIKA PROGRAM YETU)

3.TENDE (Hitajio muhimu katika Program yetu).

Jinsi ya utekelezaji wa Program hii ...

Tutakuwa katika milango ya misikiti kila siku kabla ya Swala ya Maghrib na ili kupata kuwafuturisha walio funga kama Sunna ili vyo elekeza.

Tutaanda  vijana Maalum ambao watakuwa wanafanya kazi hii chini usimamizi wa Mratibu na Msimamizi wa Jambo hili. 

Kama upo tayari kujiunga na Program hii tafadhali , WASILIANA .

+255715800772 (Whatsapp)
+255673800772
+255689604780

Kwa kutuletea Vifaa , 

Kwa walio nje ya Nchi Tafadhali tuwasiliane kwa Njia ya Whatsapp (+255715800772) Kwa maelekezo zaidi .

Na Mratibu Msimamizi , GHALIB NASSOR MONERO.

Unaruhusiwa kuituma katika Groups Mbali mbali huenda ikawa Fikra nzuri na watu wakaipenda . Mtume anasema "Mwenye kujulisha Jambo jema anapata malipo sawa na mfanyaji" kama alivyosema Mtume.

Wabilahi Taufiqh - GHALIB NASSOR MONERO L AZHARY.
Posted by MROKI On Wednesday, June 01, 2016 2 comments

2 comments:

 1. AnonymousJune 01, 2016

  MFUTURISHE NDUGU YAKO MUISLAM KWA KUFUATA SUNNA YA MTUME MUHAMMAD (REHMA ZA M/MUNGU ZIMSHUKIE JUU YAKE NA AMANI) Kwa KIPANDE YA TENDE AU MAJI

  ReplyDelete
 2. AnonymousJune 01, 2016

  Uogopeni moto, hata kwa nusu tende

  ReplyDelete

 • Facebook
 • Twitter
 • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo