Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2016

Mbunge wa Karatu Wile Qambalo.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Omary Kaang.

Na Woinde Shizza,Karatu
Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Karatu limewasimamisha kazi baadhi ya watumishi kutokana na ubadhilifu wa fedha za Umma.

Mwenyekiti wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karatu Jubilate Mnyenye amewataja waiosimamishwa ni Dr.Thobias Nkina ambaye alikuwa mganga mkuu,Judas Mahuma -Afisa Ardhi, George Ndimbo aliyekuwa Mhasibu,Jonathan Rukuntuka-Mtunza fedha,Sigfred Njanga-Mtunza fedha,Rajabu Lingoni alikuwa Muweka Hazina na Gurisha Kavuga -Mtunza stoo, wote hawa wamesimamishwa kwaajili ya uchunguzi.

Amesema kuwa kutokana na tume ya uchunguzi iliyoundwa mwezi mmoja uliopita na kamati ya fedha ya Halmashauri ,ikitaka kufahamu mapato na matumizi ya Kilimo na Afya ,ilibaini mambo kadhaa ambayo iliwasilisha kwenye.kikao kwaajili ya maamuzi,ndipo kamati ya madiwani ilipoamua kuchukua hatua ya kuwasimamisha . BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Sambamba na hayo wapo watumishi ambao wamepewa onyo ambao ni Afisa Elimu Bernad Mnyenyelwa, Dr.Kyabaroti Kyabaroti pamoja na Omari Shemdiru,ambapo wapo watumishi wengine 8 ambao wanapaswa kurudisha fedha walizozichukua shilingi milioni 81 kama masurugu ya kufanyia shughuli mbalimbali za idara zao ndani ya siku 14.

Kwa maelezo ya baraza la madiwani limeomba wizara inayohusika kwa mkutugenzi huyo imuwajibishwe kwa kuisababishia Halmashauri hasara ya milioni 800 na kushindwa kuwasimamia watumishi wake na huku miradi ya kilimo na Afya ikiathirika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Moses Mabula amesema kuwa alipohamia katika.Halmashauri    ya Karatu mwaka 2013 alikuta zimetumi zaidi ya milioni 200 pia ameongeza kuwa Halmashauri iliazima fedha kwaajili yakutekeleza miradi ya dharura,kati ya miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa stendi kuu ya Karatu,Zahanati ya Ayalabe iliyoungua moto,Ujenzi wa.madarasa 4 katika.shule ya msingi Ayalabe ili kupisha chuo ,ukamilishaji wa mitaro katika jengo la.halmashauri,ujenzi wa mahabara Endara na Mang'ola,Ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Manusway,Ukamilishaji wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Kansay .

Hata hivyo Moses Mabula amesema kuwa fedha zote ziliripotiwa katika baraza lililopita la madiwani 2015,pia amesema.ameyapokea.malalamiko yote na atawajibu baraza namna fedha zilivyotumika.
Posted by MROKI On Friday, May 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo