Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2016

 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (aliyesimama) akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (aliyesimama)  akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kushoto Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal.  

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (aliyesimama)  akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kushoto Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (Wapili kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili kulia) wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakulima wadogo waliohudhuria warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Na Mwandishi Wetu,
Wakulima wa zao la mpunga wanaojishughulisha kilimo cha umwagiliaji katika Kijiji cha Mkula wilayani Kilomberowamefanikiwa kupata mkopo wa 890Mn kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga.

Hayo yaliwekwa bayana na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal wakati wa warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Bw. Paschal alisema lengo la mkopo huo unaowanufaisha zaidi ya wakulima 350 ni kuongeza tija na uzalishaji wa mpunga ili Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na  kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

“Mkopo huu na mengine tunayotoa imelenga kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika  kilimo nchini,” alisema Bw. Paschal.

Kwa mujibu wa Bw. Paschal  mkopo huo utasaidia shughuli mbalimbali za utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mpunga pamoja na kuwezesha upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na madawa.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Benki imetoa mkopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye  ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya usindikaji wa mpunga ili kuongeza thamani wa zao hilo.

“Tunaamini mkopo huu utachagiza kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula na Pato la Taifa kutokana kuongezeka kwa tija na uzalishaji hivyo kuwa chachu ya ongezeko la thamani, ukuaji wa viwanda vya mazao ya kilimo hivyo kuchangia kuongezeka kwa ajira nchini,” aliongeza.  

Akizungumzia mikakati ya TADB kwa sasa, Bw. Paschal alisema Benki imejipanga kutoa mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa kutumia njia mbalimbali. 

Mbinu hizo zinajumuisha pamoja na mambo mengine; mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo; kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.

“Kwa kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mboga mboga, kilimo cha bidhaa za viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu. Benki pia inajitahidi kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye kuendeleza kilimo,” alisema.

Warsha hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe ambaye alitoa rai kwa Wakulima wote waliopata fursa ya kuhudhuria warsha hiyo kujipanga katika kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na TADB.

Mhe. Gembe zingatia mada zilizowasilishwa ili waweze kunufaika na Benki hii na shughuli zinazotolewa na Taasisi zingine za serikali.

“Nawasihi mrudishe mikopo mtakayopewa kwa wakati ili wakulima wengine waweze kunufaika zaidi na Benki hii na vile vile kuwezesha Benki kutoa huduma kwenye maeneo mengine ya Tanzania,” alisema.
Posted by MROKI On Wednesday, May 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo