Nafasi Ya Matangazo

May 12, 2016

MAZIKO ya mtoto wa Muhidini Issa Michuzi, Marehemu  Maggid Muhidin Michuzi (pichani) aliyefariki Mei 8, 2016 huko Afrika ya Kusini alikokuwa masomoni yamepangwa kufanyika Jumamosi Saa 10 kwemmakaburi ya Kisutu jijini Dar.

Mwili wa marehemu unatarrajiwa kuwasili kesho Ijumaa na Emirates kutokea Dubai ambako unapitia na kulala leo. Usafiri wa moja kwa moja wa Durban-Dar es Salaam umeshindikana na ndio sababu ya kuchelewa kuwasili.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mama wa marehemu, Tegeta Wazo Hill.

Ratiba itaanza Saa 4:00 Asubuhi siku ya Jumanosi hapo hapo nyumbani kwa mama wa Marehemu Kota za Wazo Hill Cement, kisha msafara wa kuelekea makaburini kupitia Msikiti wa Maamur Upanga utaanza.

Ankal na familia yake wanatoa shukrani sana kwa upendo na faraja mnaoendelea kuwapatia wakati huu mgumu.

NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement Wazo, mbele mkono wako wa kulia utaona Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona uzio wenye rangi ya njano umeandikwa Twiga Cement, unakatisha hapo upande huo huo wa kulia. ukikatisha tu utaona kuna mtaa mwingine unaingia upande wa kulia, uache na usogee mbele, utaona mtaa mwingine unaingia kulia, ingia nao huo na utakuwa umefika msibani.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.
Posted by MROKI On Thursday, May 12, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo