Nafasi Ya Matangazo

May 12, 2016

Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya  Murhandziwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa na mchezo wa Bahati Nasibu ya Taifa itakayoendeshwa na kampuni hiyo nchini  katika hoteli ya SeaCliff jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa  ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Abbas Tarimba  (kulia) na wadau wengine wa michezo ya kubahatisha wakisikiliza maelezo ya Professa Khumalo.
****************
BODI ya michezo ya Kubahatisha nchini (GBT) na kampuni ya Murhandziwa Limited, ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Naibu ya Taifa leo imetangaza kuwa maandalizi ya kuanza michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa yamekamilika na tiketi zitaanza kuuzwa nchini katika mikoa yote kuanzia Mei 21 muda wa saa 12 asubuhi.
 
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya  Murhandziwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo, amesema wakati umefika kwa wachezaji wa michezo ya kubahatisha  nchini ambapo wataweza kushiriki katika michezo hii katika mazingira ya uendeshaji wa kitaalamu na weledi mkubwa ambao utawanufaisha wananchi watakaobahatika kujishindia zawadi na kubadilisha maisha yao. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Alisema tiketi za kushiriki bahati nasibu zitauzwa kwa shlingi 500 na zitapatikana kwa mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washiriki wa mchezo wa bahati nasibu  ya taifa wanatakiwa kuwa  na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea. “Droo ya kwanza kubwa ya mchezo huu itafanyika Mei 28  mwaka huu na droo nyingine zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi.”Aliongeza Profesa Khumalo.
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Abbas Tarimba amesema kuwa ushiriki katika michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa  unachangia jitihada za serikali za kuwainua wananchi wake kiuchumi na ndio maana kuna michezo hii na inaruhusiwa kuendeshwa nchini.
 
Ujio wa kampuni  hii ya Murhandziwa Limited kumeelezwa na Professa Khumalo kuwa mbali na kuwanufaiha washindi binafsi pia utatoa ajira Zaidi ya 1,000 nchini za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kudai kuwa kwa sasa tayari wameajiri wafanyakazi 40 na idadi itaongezeka hadi 120 ambapo pia kutakuwepo na idadi ubwa ya mawakala wa kuuza tiketi nchini kote.
 
Pia imeelezwa kuwa kampuni  itabadilisha sura ya mchezo huu kwa na viwango vya kimataifa kutokana na uzoefu wake na ubunifu pia wafanyakazi wake watapatiwa mafunzo ya uendeshaji michezo hii kwa viwango vya kimataifa.

Kuhusu kukuza uchumi wa nchi imeelezwa kuwa Murhandizwa itafanya biashara na watanzania zaidi ya 200 ambao wataiouzia bidhaa mbalimbali na mara uendeshaji wa michezo ukianza matarajio ya kampuni ni kuchangia dola za kimarekani zipatazo 40 milioni katika uchumi wa taifa.

Pia uendeshaji wa michezo hii umeelezwa kuwa utanufaisha watanzania wanaoendesha biashara mbalimbali watakaokuwa mawakala wake.

Imeelezwa kuwa taratibu za uendeshaji michezo ya Bahati nasibu ya taifa itafuata kanuni na taratibu zote za nchi chini ya usimamiz wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha ambapo  Mkurugenzi wake Mtendaji wake Abbas Tarimba alisema kuwa serikali itahakikisha kanuni na taratibu za kuendesha mchezo huu zinazingatiwa na kuwataka wananchi kujitokeza kushiriki na kusisitiza kuwa ushiriki wao utawawezesha wenye bahati kujishindia zawadi kila wiki na kubadilisha maisha yao wakati huo huo kuchangia  mapato ya serikali kwa njia ya kodi.
 

Maelezo zaidi  ya mchezo yanapatikana katika tovuti ya www.bahatinasibuyataifa.co.tz na habari na matangazo kuhusiana na mchezo yatakuwa yanatolewa kwenye vyombo vya habari nchini.
Posted by MROKI On Thursday, May 12, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo