Nafasi Ya Matangazo

May 30, 2016



Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine wa tatu.

Rais Magufuli amemteua  Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo  Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi,Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Uteuzi wa  Anne Semamba Makinda   umeanza tarehe 25 Mei, 2016.

Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. 

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.

Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.
Posted by MROKI On Monday, May 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo