Nafasi Ya Matangazo

May 23, 2016

Mbunge  wa  jimbo la Iramba Bw Mwigulu  Nchemba  wa  pili  kushoto  akikabidhi bati  zaidi ya 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba  za walimu ,zahanati na nyumba  vya madarasa
Wananchi  wa   jimbo la  Iramba  wakimpongeza mbunge wao Bw Nchemba kwa  utekelezaji wa ahadi zake
Na MatukiodaimaBlog 
MBUNGE wa  jimbo la  Iramba wilayani Iramba mkoani Singida Bw Mwigulu Nchemba  ameendelea  kufanya mikutano ya  kuwashukuru  wananchi  wake  kwa  kumchagua  kwa  kishindo  katika  uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa  kutekeleza ahadi  mbali mbali  alizopata kuwaahidi  wakati wa kampeni .

Mbunge Nchemba  amekabidhi  bati  hizo  jana  wakati wa mikutano yake ya  kuwashukuru  wananchi wake wa  jimbo la Iramba kwa kumchagua na kuanza utekelezaji wa ahadi  zake.

Alisema   kuwa  lengo la  kuanza  kukabidhi ahadi  zake ni  kuwafanya wananchi kuharakisha  ukamilishaji wa  shughuli za kimaendeleo jimboni hasa katika nyanja ya  elimu  na afya  na kuwa  bati  hizo  zitasaidia  ujenzi wa vyumba  vya  madarasa ,nyumba za  walimu na  Zahanati  .

Kwani  alisema ndoto  yake ya mbeleni   ni kuona jimbo la Iramba na  wilaya ya Iramba  inaendelea  kuwa mbele katika ubora wa vyumba  vya madarasa na  wengine  kufika  kujifunza Iramba


Hivyo  alisema pamoja na  kuchangia  bati  kwa  ajili ya ujenzi  huo bado atajitolea  kununua  tofari  za  kujengea ambazo kwa  kila kijiji  vijana  watafyatua na yeye atazinunua kwa  bei ambayo  wao  watataka  kama  sehemu ya  kutoa ajira kwa vijana  vijijini pia vifaa vyote  vya  viwandani kwa ajili ya ujenzi wa miradi hiyo  ni juu yake wananchi wanachotakiwa kufanya ni  kushiriki katika shughuli za  kimaendeleo .


Pia  aliwataka  walimu na  watumishi  wanaopangwa  kufanya kazi katika  wilaya  ya  Iramba  kujenga  utamaduni wa kupenda  kufanya kazi katika wilaya  hiyo  badala ya  kuripoti na kuondoka .
Nchemba ambae ni waziri wa  kilimo ,mifugo na uvuvi  alisema  kuwa vipaumbele  vyake  kwa  wananchi wake ni maji na umeme ambavyo tayari umeme  umeanza  kusambazwa  vijijini  pia maji anaendelea  jitihada japo  alisema suala la Miundombinu bado ni  changamoto .

Wakati  huo  huo waziri Nchemba ameshauri  uongozi wa Halmashauri  kuruhusu  wanafunzi wanaopata matatizo ya ugonjwa wakiwa shuleni  kupatiwa matibabu ya  bure katika  vituo  vya afya ,Hospitali na zahanati katika  jimbo  hilo  badala ya  kuwarudisha  nyumbani .


Alisema kuna haja ya Halmashauri  kupitia  vyanvzo  vyake  vya ndani  kusaidia  kuwalipia matibabu   wanafunzi hao na kuwa  ofisi yake  itasaidia   kufidia pesa  hizo kwa  kugharamia baadhi ya  miradi ambayo inapaswa  kutekelezwa na Halmashauri kama ambavyo anafanya sasa kwa kujitolea kujenga vyumba vya madarasa na  Zahanati .
Posted by MROKI On Monday, May 23, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo