Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2016

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi, Stella Kahwa (kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu madhara ya ufungashaji batili wa mazao (LUMBESA) katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani ambayo huadhimishw akila mwaka ifikapo Mei 20,
 MKuu wa Kitengo  cha Sheria Wakili Mosses Mbunda akijibu maswali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Sheria ya Ufungashaj iwa Bidhaa
MADA: YATAMBUE MADHARA YA UFUNGASHAJI BATILI ILI UYAEPUKE NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI
A. UTANGULIZI
Ndugu waandishi wa habari;   
Wakala wa Vipimo ni Taasisi ya Serikali inayosimamia vipimo vyote vitumikavyo ki-biashara  Tanzania (Bara) kwa kuhakikisha vinakuwa sahihi. Pia  Kuhakikisha kuwa bidhaa zote zilizofungashwa zinafungashwa kwa usahihi.

Ili kuhakikisha kuwa wananchi wanafanya biashara au wanafungasha bidhaa zao kwa kutumia vipimo sahihi, Maafisa Vipimo katika kila mkoa  hufanya ukaguzi kuhakikisha kwamba vipimo vyote vinavyotumika au ufungashaji wa bidhaa  unaofanywa ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura 340 (mapitio ya mwaka 2002).

Tanzania kupitia Wakala wa Vipimo ni  mwanachama wa Shirika la vipimo Duniani (OIML), hivyo  kila mwaka ifikapo Mei 20  huungana nchi zingine na mashirika mengine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Vipimo.  Kauli mbiu ya mwaka huu (2016) ni ‘Measurements in a Dynamic World’ BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Pamoja na huduma zake nyingi inazotoa Wakala wa Vipimo, kwa leo tutazungumzia madhara ya ufungashaji batili wa bidhaa (LUMBESA) /mazao ya kilimo na misitu ambayo yanafanywa na baadhi ya wafanyabiashara/ wafungashaji kwa ajili ya kujipatia faida zaidi.

Kutokana na agizo la Mh. Waziri Mkuu alilolitoa tarehe 23/3/2016 lililoagiza Wakala wa Vipimo  Kuhakikisha inasimamia na kuhakikisha ufungashaji  batili ( Lumbesa) unatokomezwa.
Wakala wa Vipimo inashirikiana na Taasisi zingine za serikali, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya, Halmashauri za miji, vyombo vya usalama n.k. ili kuhakikisha azma inafanikiwa.

Baada ya utangulizi huo, Wakala wa Vipimo inapenda kuwafahamisha kuwa baada ya kutolewa elimu kuhusiana na ufungashaji kwa mtindo wa Lumbesa kwa sasa  tumeanza zoezi maalum la kuzuia uuzaji/ufungashaji wa mazao kwa mtindo huo.

Ufungashaji batili ni nini?
Ufungashaji batili ni ufungashaji kinyume na Sheria ya Vipimo Sura 340 Mapitio ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni zake.

  Lumbesa ni nini?
Lumbesa ni  ufungashaji batili wa bidhaa ndani ya kifungashio kwa uzito zaidi ya ule unaokubalika Kisheria au kwa kuunganisha kifungashio.
Mazao yanatakiwa  yauzwe kwa kutumia vipimo sahihi ( wapime kwenye mizani  na siyo kwa  kufanya makadirio).

Baadhi ya Matokeo ya Ufungashaji Lumbesa
  •      Kumpunja mkulima
  •      Halmashauri kukusanya mapato pungufu
  •     Kuathiri afya na maisha ya wabebaji
  •     Kuathiri nguvu kazi ya Taifa
  •     Kusababisha migongano katika jamii


Sheria inasemaji kwa wafungashaji wasiotumia vipimo sahihi
Mtu yeyote atakaye fungasha, uza, safirisha, au kuonyesha bidhaa kwa nia ya kuziuza zilizofungashwa kinyume cha Sheria ya Vipimo Sura 340 Mapitio ya Mwaka 2002 na Kanuni zake, atakuwa ametenda kosa la jinai na ataadhibiwa kwa mujibu wa Sheria.

Matokeo ya zoezi maalum tangu  4 April – Mei 18/2016
Katika kusimamia ufungashaji sahihi wa mazao Wakala wa Vipimo inafanya zoezi maalum la ukaguzi wa ufungashaji batili wa mazao (lumbesa) na tangu tarehe 4 Aprili  hadi Mei 18/ 2016,  wakosaji  1172 walififilishwa na kulipa  faini ya takriban Tshs.123m ikiwa ni adhabu  ya kutokufungasha kwa usahihi.



WITO WETU
Wakala wa Vipimo inasisitiza matumizi ya vipimo sahihi na ufungashaji sahihi katika Biashara.

Aidha, maagizo aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri Mkuu Bungeni jana, tarehe 19 Juni, 2016, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo; ambapo aliwaagiza Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutumia Kamati za ulinzi na Usalama na Watendaji Kata na Vijiji kuhakikisha wanapambana na Wafanyabiashara wenye kujihusisha na ufungashaji huo batili imezidi kutilia mkazo suala hili.

 Hivyo, tunaahidi kuongeza juhudi na maarifa katika kuhakikisha suala la lumbesa linakuwa historia hapa nchini. 
Posted by MROKI On Friday, May 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo