Nafasi Ya Matangazo

May 17, 2016

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam  pamoja na  Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 10 kuanzia saa 5 asubuhi Jumanne, Tarehe 17/05/2016.

Sababu za kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Chini ni kuzuia uvujaji uliotokea mtamboni kwenye bomba la inchi 72.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es salaam kukosa Maji:

MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE) 

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
Posted by MROKI On Tuesday, May 17, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo