Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2016

Na Joseph R  Mkonyi.
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco), limeendelea na operesheni yake maalumu ya kukagua makazi pamoja na viwanda kwenye maeneo mbalimbali ya jiji ilikutambua wezi wa Maji ndipo walipo baini wizi mkubwa wa Maji kwenye eneo la kata ya Mchikichini mtaa wa Ilala kota jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwenye eneo la tukio  Afisa biashara wa Dawasco Ilala Deogratius Ngwandu amesema kuwa wamebaini wizi wa Maji nyumbani kwa bwana Amini Idd ambapo alichepusha bomba la Maji lisipite kwenye Mita hivyo alikuwa akitumia huduma ya Maji bure na pia alikuwa akiuza Maji kwa wakazi wenzake kwa bei ya shilingi 200 kwa ndoo bila kibali, hivyo wamemkamata na kumfikisha polisi kwa hatua za kisheria.

“Tukiwa tunaendelea na operesheni yetu ya kubaini wizi Maji kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam tumeweza kumkamata bwana Amini Idd wa kata ya Mchikichini mtaa wa Ilala Kota akiwa amejiunganishia Maji kwa kuchepusha bomba lisipite kwenye mita na kutumia Maji hayo bure na kuuza kwa wakazi wenzake pamoja na matumizi yake binafsi hivyo kulikosesha Shirika mapato lakini tunampeleka polisi kwa hatua za kisheria”, alisema Ngwa’ndu.

Kwa upande wa mtuhumiwa bwana Amini Idd amekiri kuchepusha bomba la Maji lisipite kwenye mita nakuunganisha moja kwa moja kwenye bomba pamoja naukuza Maji bila kibali kutoka Dawasco ila amedai kuwa alifanya hivyo kutokana na hali ngumu ya maisha nakuomba Dawasco msamaha pamoja na kuwasihi wananchi wengine wasiibe Maji kwa kujiunganishia kinyume cha utaratibu.

“Ni kweli nilichepusha bomba la Maji lisipite kwenye mita ilikukwepa gharama nakuuzia wakazi wenzangu bila kibali kutoka Dawasco kwasababu ya hali ngumu ilikuwa najitafutia riziki ila naomba msamaha, kitendo nilichokifanya nikinyume na sheria pia nawasihi watu wengine wanaotumia Maji ya Dawasco kwa wizi waache kabla hawajakamatwa”, alisema Idd.

Dawasco inaendelea kuwasihi wakazi wote wa jiji la Dar es salaam waliojiunganishia Maji kiholela kujisalimisha iliwaweza kutambulika kwani operesheni ya kubaini wizi wa Maji ni endelevu kwa maeneo yote ya jiji la Dar es salaam hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika .


Operesheni yakubaini wezi wa Maji kwenye maeneo yote ya jiji la Dar es salaam ni agizo la waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Geryson Lwenge pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda kwa Dawasco .
Posted by MROKI On Monday, April 11, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo