Nafasi Ya Matangazo

April 27, 2016




Mwanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.
************
WANAHARAKATI WA Mtandao wa kijinsia (TGNP) wamepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), kutokana na Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na Dawasco za kuboresha huduma ya Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii inayoizunguka.


Akizungumza katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel. Ameitaka Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika kutafuta Maji.

“Tunataka kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na  jitihada tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu,  tutafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta Maji  kwani kampeni yenu ya “MAMA TUA NDOO YA MAJI KICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha.

Aidha, Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo.

 “Wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta Maji, hivi ni saa ngapi ataleta maendeleo ya nchi? Lazima tumkwamue mama katika janga hili ili na yeye aweze kujenga nchi yake” alisema Bi. Akilimali.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amehaidi hadi kufikia Disemba 31 watahakikisha kampeni ya mama tua ndoo ya Maji kichwani itawafikia wakazi wengi wa Dar hususani wale walio katika tabaka la chini.

Aidha amehaidi kutoa huduma ya Majisafi na salama bure kwa wazee, walemavu na yatima wote ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kuunganisha huduma ya Maji, pamoja na kujenga pointi za ya kunywea Maji katika sehemu mbalimbali za Jiji ikiwa ni pamoja na maeneo ya  stendi ya Mabasi ya Ubungo, Buguruni chama, Magomeni Mapipa na Kisutu stendi ya zamani.

“Mimi pamoja na menejimenti yangu tunaenda kumtua mama ndoo ya Maji kichwani mpaka kufikia mwishoni wa mwaka huu, kwani Maji yatakuwa mengi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam pamoja na Pwani” alimalizia Mhandisi Luhemeja
Posted by MROKI On Wednesday, April 27, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo