Nafasi Ya Matangazo

April 24, 2016

Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore ,akiwahutubia wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye matembezi hayo.
*************
Wafanyakazi wa TBL Group mwishoni mwa wiki walishiriki katika matembezi ya siku ya  Malaria Duniani yaliyofanyika jijini Dar e salaam na kushirikisha serikali, makampuni , mashirika mbalimbali ya serikali na yasio ya kiserikali  na wadau wengine wa sekta ya afya.

Matembezi hayo  ya kilometa tano yalianzia katika viwanja vya Green vilivyopo Oysterbay na kumalizikia katika uwanja huo TBL  ni miongoni mwa makampuni ambayo yana lengo la kuziwezesha sekta binafsi kuhimiza kuzuia na kutoa huduma za matibabu za Malaria  na kuwa na maono ya kuitokomeza kabisa.


Mratibu wa  mpango wa Afya  Bora wa TBL Group,Julieth Mgani amesema kuwa wameshiriki matembezi hayo Malaria ni moja ya vipaumbele vilivyopo kwenye mpango wa kampuni na dhamira kuu  na maono ya kampuni ni kutokuwa na maambukizi ya Malaria kabisa ifikapo mwaka 2020.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL Group wakijiandikisha kushiriki katika matembezi ya kuadhimisha siku ya Malaria.
Wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye matembezi  ya Siku ya Malaria wakimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore wakati wa matembezi ya Siku ya Malaria

Wafanyakazi wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL GROUP) wakishiriki katika matembezi

 . Baadhi ya washiriki wa matembezi ya Kilomita Tano, wakigawiwa Kinywaji cha Grand Malt.
Posted by MROKI On Sunday, April 24, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo