Nafasi Ya Matangazo

April 20, 2016

 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, Mh.Abdullah Mwinyi, (katikati-wapili kulia), akipewa maelezo na meneja wa soko la samaki Ferry, Bw.Solomon Mushi, kuhusu biashara ya samaki sokoni hapo leo Aprili 20, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wameendelea na ziara za kutembelea shughuli za kiuchumi za wananchi na leo Aprili 20, 2016 walikuwa kwenye soko la samaki la kimataifa ferry jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wakongozwa na mwenyekiti wao, Mh. Makongoro Nyerere, Wamewaeleza viongozi wa wavuvi, wakaanga samaki na wapaa samaki fursa zilizopo kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki ambapo kwa sasa lina jumla ya nchi wanachama sita, Sudan Kusini ikiwa ndio mwanachama wa hivi karibuni kabisa.

Wabunge hao pia wametembelea na kujionea shughuli zihusianazo na samaki kwenye soko hilo. Pia walipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali ya wadau hao katika soko la samaki Ferry. Soko lasamaki Ferry ni moja ya maeneo yanayotoa ajira kwa vijana wengi hapa jijini Dar es Salaam, ambao ukiacha wavuvi wao hufanya kazi ya kupaa samaki, kushusha samaki kutoka kwenye mitumbwi na kukaanga samaki. Pia kuna akina mama na baba wanaotoa huduma za chakula.

 Mh. Mwinyi, akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana mawazo baina ya wabunge hao nawashika dau kwenye soko hilo, wengine kutoka kushoto ni Meneja wa soko hilo, Bw. Mushi, Mwenyekiti wa bodi ya soko ambaye pia ni diwani wa kata ya Kivukoni jijini Dar es Salaam, Mh.Masaba, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, na Mh. Nderaikindo Kessy
 Mvuvi akieleza maoni yake mbele ya wabunge hao. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

 Shughuli za samaki zikiendelea kwenye moja ya mabanda ya soko hilo
 Mh. Makongoro Nyerere (kulia), akizungumza. Kushoto niMwenyekiti wa Bodi ya soko ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kivukoni, Mh. Masaba
 Kijana akiwa amebeba samaki wakubwa baada ya kuwatoa magamba
 Kijana akiwa amebeba samaki kuelekea mahala pa kutolea magamba
Mh. Mwinyi akipeana mikono na meneja wa soko hilo, Bw. Mushi
Posted by MROKI On Wednesday, April 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo