Nafasi Ya Matangazo

April 21, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP  Roberto Jarrin (wapili kushoto)  Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kutoka kulia) Katibu Mkuu  shirikisho hilo , Mwesigwa Selestine  (kulia) na Mjumbe wa Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa (kushoto )wakiwa kwenye picha ya pamoja  wakati walipotembelea katika ofisi za TBL Masaki  jijini Dar es Salaam.

RAIS wa Shirikisho la Soka Nchini  (TFF) Jamal Malinzi akiongoza ujumbe wa maofisa wengine wawili wa shirikisho hilo wamefanya ziara makao makuu ya ofisi za TBL Group zilizopo Masaki jijini ambapo walikutana na mkurugenzi wake Mkuu Roberto Jarrin  na kufanya naye mazungumzo.

Ziara hiyo imeelezwa kuwa ina lengo la kudumisha uhusiano miongoni mwa taasisi hizo mbili hususani katika kuendeleza mchezo wa soka nchini.
Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kulia ) Katibu Mkuu  shirikisho hilo,  Mwesigwa Selestine  (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya TFF Richard Sinamtwa (katikati)  wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Roberto Jarrin (Kulia ) wakati walipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake Masaki  jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP  Roberto Jarrin (katikati akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa ,  Kulia ni Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi
Posted by MROKI On Thursday, April 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo