Nafasi Ya Matangazo

April 25, 2016

Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group ,Lilian Makau akitoa mada wakati wa semina semina ya kuwaandaa wanafunzi  wanaosoma vyuo vikuu kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo yao  iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
 *************
Taasisi na makampuni mbalimbali mwishoni mwa wiki  yalishiriki katika semina ya kuwaandaa wanafunzi  wanaosoma vyuo vikuu kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo yao  ambayo ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kushirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.

Kampuni ya TBL Group ilishiriki katika semina hiyo ambapo Meneja wake wa kuendeleza vipaji  Lilian Makau,alitoa mada kuhusiana na jinsi ya kuhimili kufanya kazi kwenye kampuni  kubwa na zenye mifumo thabiti ya kiutendaji  na changamoto za kupata ajira.

Wanafunzi wengi pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu taratibu za ajira katika kampuni ya TBL ambapo aliwaeleza kuwa kampuni inatoa fursa za ajira kwa watanzania wote na taratibu zake za ajira ziko wazi na pia kuwa imekuwa na utaratibu wa kuajiri wasomi waliohitimu mafunzo vyuoni na kuwapatia mafunzo ya ndani na wengi wao wametokea kuwa na utaalamu wa kiwango cha juu baada ya muda mfupi kwenye ajira zao.
 Wanafunzi wakisikiliza mada na kuuliza maswali
 Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group ,Lilian Makau akitoa mada wakati wa semina semina ya kuwaandaa wanafunzi  wanaosoma vyuo vikuu kuingia kwenye ajira watakapomalizika masomo yao  iliyofanyika jijini Dar es Salaam
 wakichukua anuani ya mtoa mada 
 Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo kutoka kwa Meneja wa Kuendeleza vipaji wa TBL Group,Lilian Makau muda mfupi baada ya kumalizika semina
Posted by MROKI On Monday, April 25, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo