Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2016

Sehemu ya madawati 160 yaliyokabidhiwa na Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat katika Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam leo Aprili 4 2016.
Wanafunzi wa kidato cha kwanza na pili wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam wakimsikilza Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwahutubia wakati wa hafla ya kukabihi madawati yaliyotolewa leo Aprili 4, 2016 na Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Dar es Salaam na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwahutubia wanafunzi wa shule hiyo wakati wa hafla ya kupokea madawati 160 kutoka Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Yusuf Esack Ayub, Mjumbe wa taasisi hiyo, Ayub Abdallah (kushoto) na kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura.
Mwenyekiti wa Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat,Yusuf Esack Ayub akisaidiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kukata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 160 pamoja na vifaa mbalimbali kwaajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa Shule hiyo, Dar es Salaam leo Aprili 4, 2016 . Wanaoshuhudia ni wanachama wa taasisi hiyo, walimu na wanafunzi shule hiyo. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat, Yusuf Esack Ayub (kulia) akikabihi madawati 160 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndiyetabura kwaajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo Dar es Salaam leo Aprili 4, 2016 . Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Yusuph Mwenda, Mjumbe wa taasisi hiyo, Ayub Abdallah, Katibu wa taasisi hiyo, Ayub Esack (kushoto), waalimu na wanafunzi wa shule hiyo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mikocheni, Yusuph Mwenda (mwenye tai nyekundu) akizungumza jambo na Afisa Elimu (Taaluma) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Sunza baada ya kupokea Printer na madawati 160 kutoka Taasisi ya kidini ya Memon Jamaat kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo, jijini leo Aprili 4, 2016 . Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura.
Posted by MROKI On Monday, April 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo