Nafasi Ya Matangazo

April 14, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw. Gabriel Nderumaki.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.

Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bi. Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo.


Bi. Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)

Februari 22 mwaka huu, Bodi ya Wakurugenzi ya TSN ilimsimamisha kazi Mhariri Mtemndaji huyo kupisha uchunguzi ikiwa ni muda mfupi baada ya ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye aliyefika kwenye kampuni kuangalia utendaji na namna ya kuboresha utendaji wa kampuni. 
Posted by MROKI On Thursday, April 14, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo