Nafasi Ya Matangazo

April 27, 2016

Mkurugenzi wa Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Dk. Emmanuel Malangalila, akiwasilisha mada juu ya mradi, wakati wa uzinduzi mkoani Mbeya. Uzinduzi huo wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala, akitoa hotuba ya uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani  Mbeya

 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Munasa Nyirembe, akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Mbeya
 Mmoja wa maafisa waandamizi kutoka PS3, Dk. Conrad Mbuya, akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Mbeya
 Mtaalam wa Tafiti Tendaji kutoka PS3, Aloyce Maziku, akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Mbeya
 Mwakilishi kutoka USAID, Shanon Young, akitoa neno la salaam wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mbeya
 Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mbeya
Mratibu wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Beatha Swai, akitoa neno wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Mbeya. Kulia kwake ni Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja.
Mwakilishi kutoka USAID Shanon Young, RC wa Mbeya Amos Makala, Mkurugenzi wa PS3 Dk. Emmanuel Malangalila, na mratibu wa PS3 kutoka TAMISEMI Beatha Swai.

*****************

Uzinduzi wa Mradi wa USAID wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma Mkoani Mbeya

Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Mbeya siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.  Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Watu takribani 180 walihudhuria.  Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Mbeya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri.  

Mkoa wa Mbeya una Halmashauri saba, ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni:  Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute.  Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.  Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:

Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.

Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi.  Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.

Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi  katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.

Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.

Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa.  Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.

Posted by MROKI On Wednesday, April 27, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo