Nafasi Ya Matangazo

March 14, 2016


Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya G4S, Alfred Elia, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2016 kuhusu ushirikiano baina ya kampuni yake na taasisi ya kujitolea ya Uingereza ya Bhubesi Pride Foundation, (BPF), ambapo taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya kuunyanyua mchezo wa Raga (Rugby), pamoja na  kusaidia jamii pamoja na maendeleo mashuleni na kwenye vituo vya kijamii. Shule sita sita za jijini Dar es Salaam zitashindana katika mchezo huo Jumamosi hii jijini. Wengine pichani, ni Meneja mradi wa BPF, Mark Cole, (kulia) na Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S, Paul Fullers.Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika jana Machi 14, 2016 
 Mkutano na wahanhabari ukiendelea
 Wanahabari wakisikiliza kilichokuwa kikizungumzwa
Alfred Elia, akiwatambulisha wageni wake. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
TAASISI ya kujitolea ya Uingereza ya Bhubesi Pride Foundation (BPF) kwa kushirikiana na kampuni ya ulinzi ya G4S ya jijini Dar es Salaam, inaendesha mpango wa kuunyanyua na kuuendeleza mchezo wa Raga, (Rugby), kusaidia jamii pamoja na maendeleo mashuleni na kwenye vituo vya kijamii.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya G4S barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2016, Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko cha G4S, Alfred Elia, amesema, tayari mafunzo hayo yamefanyika jijini Arusha na sasa yako hapa jijini Dar es Salaam na yameanza rasminleo Jumatatu Machi 14, 2016 ambapo jumla ya shule sita za msingi ziko kwenye mpango huo.
Amezitaja shule hizo kuwa ni pamoja na shule ya msingi, Mapambano, Makumbusho, Hananasifu, Victoria, Mugabe na Shekilango.
Kwa upande wake, Meneja wa BPF, Mark Cole, alisema, mpango huo unaendeshwa kwenye nchi mbalimbai za Afrika na ni wa mwaka mmoja. “Tayari tumefanya mafunzo haya nchini Uganda, Kenya, Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia, Botswana, Namibia na Afrika Kusini, alisema Cole
Alisema, nia ya mpango huo ni kuunganisha jamii kupitia raga, kuelimisha thamani na stadi za maisha, pamoja na kunyanyua uwezo wa walimu nchini, kulea viongozi wa jamii, wake kwa waume pamoja na kuweka uwezeshaji huu kuwa endelevu.
Maendeleo ya matokeo ya muda mrefu kupitia miradi inayoonekana, mfano kupanda miti, kwa kushirikiana na wabia wetu katika nchi tajwa.
Tayari shirika hili kwa kushirikiana na G4S Tanzania limeishafanya haya Arusha na Moshi ambapo watoto zaidi ya watoto 600 wa mikoa hio walipata mafunzo ya raga pamoja na stadi za maisha ambapo pia G4S ilipanda miti katika maeneno mbalimbali
Naye Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S, Paul Fullers, alisema, G4S kwa kutambua masuala ya usalama, ndio maana imeamua kushirikiana na BPF ili kujenga uelewa miongoni mwa wanafunzi kuhusu masuala ya usalama wawapo shuleni, mabarabarani na hata nyumbani.
“Mafundisho haya yanafanyika kila mwaka kuanzia mwezi January mpaka Julai, ambapo shuguli za kijamii hufanyika sambamba na makampuni yanayojitolea kudhamini- G4S Africa, akiwa ni mdhamini mkuu na muhimu kwa hii taasisi.” Alifafanua Fullers.
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs). Vyama vya raga kitaifa, idara mbalimbali za kiserikali, shule za kimataifa pamoja na makampuni mbalimbali kwenye jamii husika, kuongezea thamani katika huu uhusiano pamoja na kujengea uwezo, alisema.



 Mark Cole, Meneja mradi wa BPF
 Finn Sims, Meneja anayehusika na vyombo vya habari wa BPF
 Paul Fullers, Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S
Posted by MROKI On Monday, March 14, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo