Nafasi Ya Matangazo

February 24, 2016

Afisa huduma kwa wateja wa Airtel , Juma Hassan akitoa maelezo ya jinsi ya kupata huduma mbalimbali za kisasa kwa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars walipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo liliko Morocco jijini Dar es Salaam
 Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakimfatilia kwa makini Afisa Afisa wa huduma kwa wateja wa Airtel Bw Stephen Makongoro  wakati alipokuwa akitoa maelezo ya huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Twiga Stars ilitembelea duka jipya la Airtel Expo lililopo jijini Dar es salaam
Baadhi Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakitumia vifaa mbalimbali pamoja na simu za kisasa zilizopo katika duka la Airtel Expo wakati timu hiyo ilipotembelea duka hilio Jana, akishuhudia ni Afisa huduma kwa wateja wa Airtel , Boaz
 Kikosi kizima cha timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars pamoja na uongozi wa timu hiyo na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati timu hiyo ilipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo lililopo Morocco jijini Dar Es Salaam
 Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Adriana Lyamba (nyuma) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars ambao wametokana na matunda ya mpango wa kuinua soka la vijana chini ya miaka 17 wa  Airtel Rising Stars.
Baadhi Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars wakitumia simu zilizopo ndani ya duka la Airtel Expo kupiga selfie na kuona ubora wa simu hizo wakati walipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo liliko Morocco jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba akimkabithi  simu mmoja ya wachezaji wa timu ya wanawake ya Twiga Stars , Maimuna Hamisi mara baada ya kujibu maswali juu ya huduma na bidhaa za Airtel kwa ufasaha  
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba akimkabithi  Meneja wa Timu ya Twiga Stars , Furaha Francis Modem aina ya Airtel wingle inayounganisha watumiaji zaidi ya 10 na huduma ya Wifi itakayosaidia kikosi hicho kuunganishwa na huduma za intaneti wakati wote.  Modemu hiyo ilikabidhiwa wakati Airtel ilipotembelea duka la kisasa la Airtel Expo lililopo Morocco Jijini Dar es Saalam
Posted by MROKI On Wednesday, February 24, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo