Nafasi Ya Matangazo

October 09, 2015

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA, Bw. Focus Mauki (kushoto) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi ya Mfumo mpya wa malipo wa Kelektroniki kulipia huduma za Bandari. Mfumo huo wa malipo tayari umeanza kutumika tangu mwezi Julai mwaka huu na umeongeza ufanisi wa Bandari na kurahisisha kazi ya kutoa mizigo Bandarini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA wa Mamlaka, Bw. Kilian Challe na Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Frank Mvungi.

Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA wa TPA, Bw. Kilian Challe akiwaeleza Waandishi wa Habari kuhusu mipango ya Mamlaka kuanza kutumia huduma za simu za mkononi, Master Card na Visa kulipia gharama za Bandari kwa kupitia mfumo wake mpya wa Malipo kwa njia ya Kielektroniki (IePS). Kushoto ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi TPA, Focus Mauki na Afisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo, Bw. Frank Mvungi.
                                                                         ************

Na Focus Mauki-TPA
Wateja wa Bandari ambao ni Mawakala wa kutoa mizigo Bandarini sasa wataanza kutumia huduma za malipo kupitia njia za Simu za Mkononi, Visa Card na Master Card wakati wa kulipia gharama za huduma Bandari.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Kilian Chale wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Ijumaa, Oktoba 9.

“Napenda kuwatangazia wateja wetu na Watanzania wote kuwa katika siku za karibuni Mfumo wetu wa Malipo kwa njia ya Kielektroniki (IePS) ambao tuliuzindua Julai 2015 utaanza kuruhusu matumizi ya Master Card, Visa na simu za mkononi katika kulipia huduma za Bandari,” amesema Kilian.

Kilian ametoa wito kwa Mawakala wa Mizigo Bandarini kuendelea na usajili wa ktumia mfuo huu ili kurahisisha na kuharakisha kazi ya kutoa mizigo Bandarini na kuongeza ufanisi wa Bandari katika kuhudumia wateja wake.

Tayari Mawakala wengi wameanza kutumia mfumo huu ambao tayari umeeunganishwa na Benki za CRDB, NMB na Benki ya Posta ili kumwezesha Wakala kupata Ankara ya malipo, kufanya malipo na kisha kwenda moja kwa moja katika eneo la kuchukulia mzigo ndani ya Bandari.

Mpaka sasa Wakala anaweza kutumia Benki ya CRDB na NMB kufanya malipo kwa kutumia CRDB Sim Banking, CRDB Internet Banking, CRDB fahari Huduma, NMB Internet Banking, NMB Mobile Banking na pia anaweza kutumia matawi ya CRDB, NMB na Benki ya Posta.

Ili kuweza kutumia mfumo huu wakala anapaswa kusajiliwa na Mamlaka na baada ya kusajiliwa anaweza kuingia katika mfumo kupitia tovuti rasmi ambayo ni www.tpapayments.com.

Mteja wa kawaida pia anaweza kuingia katika tovuti hii na kuweza kuona Ankara ya malipo ya huduma za Bandari kwa kila mzigo au gari aliloagiza. Pamoja na mambo mengine mfumo huu unatarajiwa kuweka uwazi na kupunguza kwa kiwango kikubwa malalamiko ya wateja ya kukosa  taarifa sahihi za gharama za mizigo yao.
Posted by MROKI On Friday, October 09, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo