Nafasi Ya Matangazo

October 07, 2015

Meneja Mwandamizi wa  Biashara Ndogo na Kubwa  wa Benki ya DCB, Haika Machaku akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuwapatia shuhulisho la masuala ya kifedha wateja na kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara zao  ameyasema hayo leo katika hafla ya kusherekea wiki ya huduma  kwa wateja iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa Technolojia ya Habari na mawasiliano Mohamed Mtulia
.Meneja Masoko wa Benki ya DCB,Boyd Mwaisame akisisitiza jambo katika hafla ya kusherekea wiki ya huduma  kwa wateja, kulia ni Meneja Mwandamizi wa  Biashara Ndogo na Kubwa  wa Benki ya DCB, Haika Machaku.
Meneja Mwandamizi wa  Biashara Ndogo na Kubwa  wa Benki ya DCB, Haika Machaku akikata keki na wateja wa Benki hiyo katika hafla ya kusherekea wiki ya huduma  kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo leo jijini Dar es Salaam. 
************ 
WAJASIRIAMALI nchini wametakiwa kuacha kuhofia kuchukua mikopo  katika benki mbalimbali kwa kuogopa kutozwa riba kubwa.

Hatua inakuja kutokana na kuonekana bado kuna idadi kubwa ya wajasiriamali wanaobuni bidhaa mbalimbali lakini wanakwama kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha wa kuendeleza biashara zao.

Akizungumza jijini hapa leo na waandishi wa habari, meneja mwandamizi wa biashara ndogo na kubwa, kwa niaba ya mkurugenzi msaidizi wa Benki ya biashara ya Dar es salaam (DCB), Haika Machaku, amesema kuwa wajasiriliamali wanatakiwa kujijengea desturi ya kuchukua mikopo ili kujiendeleza katika shughuli za kimaendeleo.

“Tunaahidi kuwapatia shuhulisho la masuala ya kifedha ambao situ katika kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara zenu lakini pia kuwahamasisha ninyi kufanikiwa zaidi hivyo katika wiki hii ambayo ni ya huduma kwa wateja tunakataka wajasiriamali ”amesema Machaku.

Aidha amesema kuwa katika wiki hiyo wanatarajia kutoa huduma mbalimbali sambamba na kusikiliza maoni ya wateja kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.

“Lengo letu siku zote ni kutoa huduma bora kewa haraka na zenye kukidhi matakwa ya wateja lakini katika huduma tutakazozitoa ni pamoja na kuendeleza huduma ya mikopo ya nyumba na uboreshaji wa nyumba” alisema.
Kwa mujibu wa Machaku amesema mwaka huu wametenga takribani billion 86 kwa wateja wote kwaajili ya kuwakopesha ili kuwawezesha kukuza biashara zao na kuongeza kuwa hadi sasa wameshafungua matawi nane katika sehemu mbalimbali. Source:Michuzi Media.
Posted by MROKI On Wednesday, October 07, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo