Nafasi Ya Matangazo

July 06, 2015

Meya wa Ilala, Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo. Pamoja nae ni Mbunge wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa NEC wa CCM,
Diwani wa  kata ya  Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa akihutubia wananchi katika uwanja wa shule ya msingi kitunda mwishoni mwa wiki ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na kukamilisha ahadi mbalimbali alizokuwa amezitoa.
Mmoja wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya wenzake  kutoka kwa Meya wa Manispaa ya ilala  ambazo alikuwa amewaahidi wakati wa mkutano wa  Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
Baadhi ya madiwani na wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya Jerry Slaa kwa kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga
 Watoto wakitoa burudani wakati wa mkutano huo
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba ya Meya Jerry Slaa
Baadhi ya madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.
Posted by MROKI On Monday, July 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo