Nafasi Ya Matangazo

July 18, 2015

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilakiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrer Mngereza alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015. Marehemu Banza Stone, aliyefariki jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu,  amezikwa jioni hii katika makaburi ya Sinza. Marehemu Banza Stone atakumbukwa kwa umahiri wake wa utunzi na uimbaji alipokuwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta, Tot na Extra Bongo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika  alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa Katibu wa bendi ya TOT, Gasper Tumaini, ambako marehemu Banza Stone aliwahi kufanya kazi enzi za uhai wake
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole kaka wa marehemu alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa wana familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji mama mzazi wa marehemu  katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na kiongozi wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta Asha Baraka  katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu   katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na  Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu   katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu  Ramadhani Masanja "Banza Stone" likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
 Waombolezaji wakilia kwa uchungu wakati mwili wa Banza Stone ukipelekwa mazikoni
 Mama Salma Kikwete, Asha Barka na mama wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni wakati  mwili wa merehemu Banza Stone ukipelekwa mazikoni
 Mama Salma Kikwete akiagana na kiongozi na mwimbaji wa African Stars wana Twanga Pepeta ambaye alifanya kazi kwa karibu na Banza Stone tokea kuanza kwa bendi hiyo
Mama Salma Kikwete akiaga waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
Posted by MROKI On Saturday, July 18, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo