Nafasi Ya Matangazo

July 27, 2015

 Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere juu ya kuhama kwake katika chama hicho katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam. 
Mwandishi akiuliza swali kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere ambaye leo alikutana na waandishi habari juu kuhama chama hicho na kurejea CCM katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. 
**********
Na Chalila Kibuda ,Michuzi Media.
MBUNGE wa Viti  Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa  wa Mara ,Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam,Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje  bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.

“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa Chadema na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa  nasema narudi  nyumbani kutumikia”amesema Leticia.

Leticia amesema kwenda Chadema alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.


Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa  shahihi.
Posted by MROKI On Monday, July 27, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo