Nafasi Ya Matangazo

June 24, 2015

Taarifa zinazoenea katika mitandao ya kijamii ya facebook, Twitter na WhatsApp juu ya kifo cha Mwanamuziki mnguli wa Mziki wa dansi hapa nchini Ramadhani Ramadhani Masanja 'Banza Stone' sio za kweli.

Akiongea na Father Kidevu Blog mmoja wa ndugu wa karibu wa mwanamuziki Yusufu Masanja huyo amesema huo ni uzushi tu juu ya ndugu yao na Banza licha ya kuwa kweli anaumwa lakini bado yupo hai.

"Banza kweli anaumwa lakini si kweli kuwa amefariki....Banza yupo na asubuhi hii tunampeleka Hospitali ambapo ana Clinic anayohudhuria kila mwezi," alisema Masanja.

Hii ni zaidi ya mara ya pili sasa mwanamuziki huyo kuzushiwa kifo tangu anze kuugua. 
Posted by MROKI On Wednesday, June 24, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo