Nafasi Ya Matangazo

May 02, 2015

1Kijana Nassib Abdul maarufu kama Diamond Plutnumz akiwasili na mpenzi wake Zari katika Hafla iliyopewa jina “Zari All White Party” iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waalikwa na mashabiki mbalimbali wa mwanamuziki Diamond Platnumz. 

Hafla hiyo ilifana kwa kiwango cha hali ya juu na iliyomfanya Zari kulia jukwaani kwa furaha kutokana na alivyopokelewa na watanzania huku wakiita Wifi, Wifi!!, Kila aliyehudhuria katika hafla hiyo alionekana akiwa amevalia mavazi meupe na mwenye furaha.  Lakini pia hata mimi pamoja na kwamba nilienda kuripoti matukio ya hafla hiyo  ilibidi nifuate utaratibu kwa kugonga vitu vyeupe kama wengine ili nisije nikaharibu shughuli ya watu.

Nilifurahia sana hafla hiyo kama walivyofurahia mashabiki wengine wa Diamond na nitamkubali siku zote kwa kazi yake nzuri anayoifanya kimuziki  akiiweka Tanzania juu katika ramani ya muziki Afrika na Duniani “Viva Diamond, Viva Zari” Asanteni.
 2Diamon Platnumz  na Zari wakihojiwa na mtangazaji wa Clouds Media Shadee wakati walipowasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya hafla kushoto ni Meneja na msimamizi wa bendi ya Yamoto.
 21 
Ilikuwa Full Burudani kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Picha zaidi: FULLSHANGWE BLOG
Posted by MROKI On Saturday, May 02, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo