Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2015



KIPENGA cha watangaza nia wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kama kimeshapulizwa, hii ni kutokana na kasi ya hao wanaotaka kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama tawala kuanza harakati  na kutoa ratiba zao kuutangazia umma nia yao.

Wapo ambao wamesha tangaza hadharani nia yao hiyo ya kukiomba chama kuwapa ridhaa ya kuwaomngoza watanzania na pia kukiongoza chama hicho kikongwe Tanzania.

Jumamosi hii taifa lita shuhudia kada wa Chama hicho na Mbunge wa Monduli aliyepata kuwa  Waziri Mkuu, Edward Lowassa atatangaza nia yake ya kuomvba ridhaa ya chama chake kumpa nafasi ya kuwania Urais katika uchaguzi mjkuu utako fanyika Oktoba mwaka huu.

Lowassa atafuatiwa na Kada mwingine na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Charles Makongoro Nyerere nae anataraji kutangaza nia yake ya kuwaomba wana CCM wenzake kumpa nafasui ya kuwania urais akiwa Butiama.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe nae wakati wowote atafanya hivyo huko kijijini kwake Chiponda Rondo, Mkoni Lindi. Idadi ya wana CCM waliotaka kuwania nafasi hiyo mwaka huu ni kubwa na huenda kulinganisha na miaka ya nyuma.

Pia vyama vya upinzani navyo watu wengi wanaweza jitokeza kuwania nafasi hiyo, kupitia vyao na kupitia umoja wao waliouanzisha wakati wa Bunge la Katiba kuwa watasimamisha Mgombea Urais mmoja ambaye atachuana na Yule ambaye atapitishwa na CCM.

Kwa kambi ya upinzani sina tatizo napo sana na huenda wao wakawaleta wale wale wa miaka yote ambao wamekuwa wakigombea, nahapa tunataraji majina kama ya Ibrahim Lipumba, Dk Wilbrod Slaa, Freeman Mbowe, Dk Emmanuel Makaidi au hata Joseph Mbatia akaingia kwa mara ya kwanza.

CCM naweza kusema kuwa ndio watako tupa picha halisi ya uchaguzi wa mwaka huu kwa ngazi ya Urais utakuwaje. Hii ni kutokana na chama hicho kuwa na watu wengi ambao wanaweza kupitishwa na changamoto wanayokabiliana nayo mwaka huu ndani ya CCM basi naimabni wao wakimaliza uchaguzi wa  nani agombee urais basi watakuwa wamemaliza kazi na huko mbele watakuwa wanateleza tu na watabaki na vita ya ubunge.

Kubwa ambalo nataka kulisema hii leo ambalo limenijia katika mawazo yangu na kiukweli ni jambo la muhimu, ni kuacha siasa za maji taka.

Naamini wapo wagombea ambao watatumia lugha zisizo faa na ambazo hazikubaliki katika majukwaa ya kiasiasa. Hizi ni ni zile siasa za kuchafuana ambazo zinawafanya wagombea kuacha kujinadi kwa sera zao ambazo zitatupa ushawishi wa kumpigia kura na badala yake anatumia muda mwingi kutukana na kuwaponda kwa kashfa za kila namna.

Si vyema kutumia muda wako mwingi kujinadi kwa kumchafua mwenzako, maana mbali na kuzungumza majukwaani lakini teknolojia ya sasa inaturuhusi kushawishi wapiga kura wakowakuone bora zaidi hata kwa njia ya mtandao.

Sio wagombea tu lakini hata na sisi ambao tumeunda makundi au kambi kwaajili ya kumsaidia mgombea fulani ili ashinde basi tuwe wastaarabu na tuache kutumia lugha za matusi na kejeli zisizo kuwa na maana na zingine kukosa maadili ya kitanzania.

Tusitumie uhuru wetu wa kupashana na kupata habari kwa kupitiliza, uhuru huu unaweza kututia matatizoni kwani tayari Sheria ya Mkosa ya Mtandao 2015 imesha pitishwa na inaweza kutugharimu kama sio wanasiasaa basi wafuasi kutokana na lugha na posti zetu katika mitandao ya kijamii.

Leo hii ikupita katika mitandao ya facebook, Twitter, blogs na WhatsApp utashuhudia baadhi ya watu wakitoa kashfa na maneno tofauti ya kuwaponda watu fulani fulani waliotangaza nia au waliona matarajio ya kutangaza nia ya kuwania uongozi fulani.

Nadhani jambo jema la kufanya hivi sasa ni kutumia mitandao hii ya kijamii, na hata vyombo vingine vya habari kwa ufasaha na umakini kwa kunadi sera na mipango thabiti ya wagombea wetu tunaowataka na muda mwingi tuwanadi wao na si kutumia kwa kutoa kashfa na kejeli kwa mgombea mwingine ambaye unaanika mabaya yake tu kana kwamba yeye hana zuri hata moja hapa duniani.

Wagombea pia nanyi wahimizeni wafuasi wenu kuwa watulivu katika kipindi hiki cha kuelekea kupata wagombea, amani  na upendo liwe jambo jema la kusisita kila iitwapo leo maana bila hiyo ahata hilo tunalolitaka halitakuwa na raha.Porojo hii imetoka katika gazeti la HABARILEO toleo la Mei 29,2015 kama WAZO.
Posted by MROKI On Friday, May 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo