Nafasi Ya Matangazo

May 06, 2015

Mahakama Kuu ya India imemtupa jela miaka mitano Mwigizaji nguli wa Bollywood, Salman Khan baada ya kukutwa na hatia ya kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine wanne na kukimbia katika ajali ya barabarani iliyowakumbwa watu hao wasio na makazi.

Tukio hilo lilitokea mnamo mwaka 2002 katika mji wa Mumbai na kesi hiyo kudumu kwa miaka 13 hadi inatolewa hukumu yake.

Khan katika utetezi wake aliiambia Mahaka kuwa aliyekuwa akiendesha gari hilo lililowaparamia watu hao ni dereva wake na si yeye lakini Mahakama ilisema Khan ndie alikuwa akiendesha na alikuwa amelewa.

Wataalam wa sheria nchini humo bado wanatoa nafasi kwa muigizaji huyo kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Aidha taarifa zinasema Mwanasheria wa Khan, tayari amesha wasilisha hati ya rufaa Mahakama Kuu ya Bombay na huenda ikasikilizwa mapema.

Khan ni mmoja wa wacheza filamu wakubwa wa Bollywood na ameshiriki katika kucheza filamu zaidi ya 80 za kihindi.

Miongoni mwa filamu zake ni pamoja na Dabangg, Ready, Bodyguard, Ek Tha Tiger, Maine Pyar Kiya na Hum Aap Ke Hain Kaun, na ambazo zimepata mauzo makubwa duniani.
Posted by MROKI On Wednesday, May 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo