Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2015

 Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara, Abel Yiga, (kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga wakati waziri huyo alipotembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji.
 Meneja Unedelezaji wa Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, Asa Mwaipopo, (katikati), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), wakati wa ziara yake ya kutembelea mgodi wa North Mara ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Kulia ni Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto), akisalimiana na Meneja  Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, wakati alipofika kwenye kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na mgodi wa North Mara, Mara ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara Jumatatu Mei 4, 2015, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga,(Watatu kulia), Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jimmy Ijumba, (Wapili kulia) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, akizungumza na mama huyu mkazi wa kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na eeno la mgodi wa North Mara, huko Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara, wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo Jumatatu Mei 5, 2015 ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (Wapili kushoto), akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa nyumba moja kwa mtindo unaoitwa na wakazi wa Nyamongo "Tegesha", mita chache kutoka uzio wa mgodi wa North Mara, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Naibu waziri amesikitishwa na mtindo huo ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la Nyamongo, hujenga majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo kwa matarajio ya kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini iliyofanywa awali.
 Meneja wa Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, (wakwanza kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (wapili kulia), Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo, (watatu kulia) na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, unaomilikiwa na Acacia, Jimmy Ijumba, mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea maeneo yanayozun guka mgodi huo huko Nyamongo wilayani Tarime Mkoa wa Mara Jumatatu Mei 4, 2015
Wananchi wakiendelea na ujenzi kwa mtindo wa "Tegesha" mita chache kutoka eneo la machimbo (pit), la mgodi wa dhahabu wa North Mara, huko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara jana. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga, amesikitishwa na mtindo huo wa "Tegesha", ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la Nyamongo, hujenga majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo kwa matarajio ya kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini iliyofanywa awali. Naibu huyo wa waziri yuko ziarani kutembelea maeneo ya mgodi huo ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Posted by MROKI On Monday, May 04, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo