Nafasi Ya Matangazo

May 16, 2015



Mgombea usra wa chama cha Republican huko Marekani, Mitt Romney na Bingwa mara tano wa uzito wa juu wa Ngumi duniani, Evander Holyfield wamezipiga katika pambano la hisani lililofanyika katika Salt Lake City.

Romney, 68, alikutanishwa na Holyfield, 52, katika mpambano wa raundi mbili ambapo Romney alifanikiwa kumtwanga ngumi mpinzani wake na kumwangusha chini lakini baade mwanasiasa huyo aliamua kutimua mbio ulingoni baada ya Holyfield kuinuka.

Pambanao hilo lilitawaliwa na maigizo tu na mabondia hao walikuwa wakiruka ruka tu ulingoni na hata kuanguka kwa Holyfield ilikuwa ni maigizo tu.

Romney akionekana kumrushia ngumi Holyfield.
Pambano hilo lililenga kukusanya fedha kwaajili ya kuwawezesha madakrati kusaidia ufanyaji upasuaji wa macho kwa nchi zinazoendelea.
Dola za kimarekani Milioni moja zilipatikana katika harambee hiyo. 
Posted by MROKI On Saturday, May 16, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo