Nafasi Ya Matangazo

April 26, 2015


Mojawapo ya ndiga zilizoshindaniwa likioneshwa
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akiongea na Dennis Ssebo wa 97.3 EFM kwenye hafla hiyo jana katika uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akimkabidhi ndinga yake mshindi  Stella Joseph kutoka wilaya ya Ilala
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akimpongeza mshindi Gabriel Robert kutoka wilaya ya Temeke bada ya kumkabidhi ndinga 
Mojawapo ya ndiga zilizoshindaniwa
*******
Hatimaye Washindi wa shindano la Shika Ndinga la 93.7 EFM wamepatikana baada ya mchuano mkali uliofanyika jana Aprili 25, 2015 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam. 
 
 Fainali hiyo iliwahusisha washiriki 10 kutoka katika wilaya zote tatu za mkoa wa Dar-es-salaam watano kati yao wakiwa wanawake watano wakiwa ni wanaume. 
 
Shindano hilo lilihudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akiwa kama mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na Mstahiki Naibu Meya wa wilaya ya Temeke Mhe. Juma mkenga. Mhe Sadik alisema ni ubunifu wa hali ya juu ulioneshwa na kituo cha 93.7 EFM kwa kuanzisha shindano la aina yake ambalo litaongeza ajira kwa vijana na kuinua hali zao za uchumi.
 
Mkuu wa Mkoa huyo pia aliwaasa washindi kutumia ndinga walizoshinda ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa upande wake Mhe. Paul Makonda alisema vijana wajifunze kujitokeza katika mashindano kama haya maana zaidi ya kuburudisha yanabadilisha maisha yao kwa namna yatofauti. 
 
Washindi waliojishindia ndinga kwa upande wa wanaume ni Gabriel Robert kutoka wilaya ya Temeke mwenye umri wa miaka 36 na Stella Joseph kutoka wilaya ya Ilala mwenye umri wa miak 26 ambao kwa pamoja wamesema shindano halikuwa rahisi na wanafuraha kubwa ya kujishindia gari hizo ambazo watazitumia katika biashara zao.
 
Aidha wameishukuru redio ya 93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na kuwashauri wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali wasikilizaji wake.
Posted by MROKI On Sunday, April 26, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo