Nafasi Ya Matangazo

April 23, 2015

Kikosi cha FFU Oljoro ambacho kitashuka kuchuana na Tanzanite SC .
 Mkoani Arusha mwishoni mwa juma hili kunataraji kufanyika michuano ya NDONDO CUP itakayoshirikisha jumla ya timu nane kutoka mkoani hapa.

Lengo la michuano hiyo ni kuwakutanisha wapenda soka mkoa wa Arusha pamoja na kuwapa nafasi wa  mashabiki wa mchezo huo Mkoani hapa kukutana sehemu moja.

Michuano hii itaanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa ya tarehe 24/04/2015 na kufika tamati siku ya jumapili.

Mshindi wa kwanza katika michuano hii atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano (500,000) pamoja na kikombe, mshindi wa pili atajipatia fedha taslimu shilingi laki tatu (300,000).

Timu zitakazoshiriki katika michuano ya NDONDO CUP 2015 ni FFU OLJORO, TANZANITE SPORTS FOUNDATION, RED STAR, TANZANITE VETERAN, LEMARA BOYS, NJIRO SPORTS, SMALL NYOTA na UMBRELA GARDEN.

Ratiba katikIMA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO

FFU OLJORO VS TANZANITE SPORTS CLUB, TANZANITE VETERAN VS RED STAR, LEMARA BOYS VS UMBRELA GARDEN, NJIRO SPORTS VS SMALL NYOTA
Michezo yote itapigwa siku ya ijumaa kwa mfumo wa bonanza na nusu fainali itakuwa siku ya jumamosi wakati mchezo ya fainali utapigwa siku ya jumapili.

Michuano hii itafanyika katika uwanja wa AICC uliopo karibu na round about ya KIJENGE. muda ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.

Katika michuano hii kutakuwa pia na burudani toka kwa bingwa wa kucheza na baiskeli dunia (BMX CHAMPION) VICK GOMEZ, pamoja na wasanii wa Bongo flava akiwemo G NAKO, CHABA, KINGS, na mchekeshaji KATARINA.
Posted by MROKI On Thursday, April 23, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo