Nafasi Ya Matangazo

April 27, 2015




Machezaji wa vishale(Darts) wa klabu ya Friedz ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wakiwa wameshika kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Friendz walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
 *************

Na Mwandishi Wetu.

KLABU ya Friendz Wanaume yenye makazi yake Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo wa Vishale(Darts) Taifa  yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 100,000/=.

Nafasi ya pili katika mashindano hayo ilichukuliwa na klabu ya Lugalo ambayo ilizawadiwa pia Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/=.

Upande wa Wanawake timu ya Friendz yenye makazi yake palepale Tiptop Manzese ilitwaa ubingwa wa Taifa na hivyo kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 60,000/= wakati nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na klabu ya Kimanga ambao walizawadiwa kikombe na pesa taslimu Shilingi 40,000/=.

Fainali za mashinadano ya mwaka huu zilikuwa na mchezo wa mmoja mmoja(Singles) na wawili wawili (Doubles) kwa Wanawake na Wanaume ambapo upande wa Doubles Wanaume, Jemes Mlai na Sylivanus Sylivester wote wa Ibukoni klabu waliiibuka mabingwa na hivyo kuzawadiwa Kikombe na Pesa Taslimu Shilingi 120,000/=, wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na klabu ya Jemes Enea na Nungwa Sadiloa wote wa Polisi Balax ambao walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 80,000/=.

Upande wa doubles Wanawake Subira Waziri na Happiness Modaha wote wa Klabu ya Ibukoni waliibuka mabingwa na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu shilingi 60,000/= wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Fabiola Namajojo na Veronica Sule ambao walizawadiowa kikombe na pesa taslimu Shilingi 40,000/=

Upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanaume, Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo alitwaa ubingwa na kuzawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi120,000/= wakati nafasi ya pili ilichukuliwa na Jemes Enea kutoka Klabu ya Polisi Balax ambaye alizawadiwa Kikombe na pesa taslimu 60,000/=.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Selestine Onditi, aliwashukuru washiriki wote kwa moyo wa kujitoa kushiriki mashindano ya Kitaifa kutoka katika mikoa mitano kwa kujitegemea na pili aliwapongeza mabingwa waliofanikiwa na wale ambao hawakufanikiwa wakajipange kwa mwaka ujao.

Nae mwenyekiti wa Chama cha Vishale Taifa(TADA), Gesase Waigama aliwashukuru pia washiriki wote nakuwatakia safari njema za kurudi majumbani kwao pamoja na maandalizi mema kwa watakaoshiriki mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Mikoa iliyoshiriki mashindano ya Vishale Taifa mwaka huu ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Monday, April 27, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo