Nafasi Ya Matangazo

March 30, 2015

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akishiriki usafi wa mazingira katika Mtaa wa Mlalakuwa na wakazi wa Mtaa huo wakati wa operesheni maalum ya kuweka safi mazingira.
********
MPANGO wa kuweka safi mazingira ya jiji la Dar es Salaam utafanikiwa tu iwapo viongozi na watendaji watatekeleza mpango huo kwa vitendo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa operesheni maalum ya kusafisha maeneo mbalimbali ya Kata ya Mikocheni, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema umefika wakati sasa viongozi kchukua hatua za makusudi za kuhakikisha mkakati wa kuweka safi jiji unafanikiwa kwa kuwashirikisha wananchi wao kwa vitendo.

Mwenda alithibitisha hilo kwa vitendo wakati alipojumuika na wananchi mbalimbali wa Mtaa wa Mikocheni B, Manispaa ya Kinondoni kusafisha maeneo mbalimbali ya Mtaa  huo ikiwemo sehemu za mto Mlalakuwa na kuwahakikishia wananchi wake kuwa hilo litakuwa zoezi endelevu ili kuhakikisha kila mwananchi anahamasika na kuweka safi mazingira yanayomzunguka.

“Kinondoni imekuwa Manispaa ya kuigwa katika suala la usafi, na hili tunalitekeleza kwa kujumuika na wananchi wenzangu kwa ajili ya kusafisha maeneo mbalimbali na leo tupo Kata ya Mikocheni B. viongozi wanatakiwa waoneshe wananchi wao kwa vitendo, nao watahamasika .” alisema Mwenda.


 Meya wa Manispaa ya Kinondoni akioneshwa sehemu mbalimbali za Mto Mlalakuwa wakati wakiufanyia usafi.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa kwenye picha ya pamoja na wakazi wa Kata ya Mikocheni B baada ya kumaliza kufanya usafi katika mto Mlalakuwa.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kulia) akikabidhi viroba kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni B, Sixbert Thomas kwa ajili ya kuzuia maporomoko ya ardhi katika Mto Mlalakuwa, wakati wa operesheni hiyo.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa, Abraham Shoo (kushoto) wakati wa operesheni maalum ya kusafisha mazingira katika Kata za Manispaa hiyom Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Nicodemus Masika.
Posted by MROKI On Monday, March 30, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo