Nafasi Ya Matangazo

March 28, 2015

V Money
Mwana dada Mtanzania anaetikisa hivi sasa katika anga za muziki nchini na ukanda wa Afrika Mashariki Vanessa Mdee, a.k.a V Money, akimshgirikisha raoa maarufu kutoka nchini Afrika Kusini, K.O  ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina laNobody But Me

Wimbo huo uliotungwa nae Vanessa Mdee, Ntokozo Mdluli na Nahreel, unaelezwa kuwa ni miongoni mwa nyimbo nzuri ambazo zinachezeka Club.

Huu ni wimbo wa tano wa mwana dada huyo ukifuatiwa na ule wa Siri, lakini hii ni mara ya kwanza kwa mana dada huyo kuachia Video na singo hiyo kwa wakati mmoja.
Wimbo huo wa  Nobody But Me umeandaliwa na mwaandaaji wa muziki  Nahreel, wa Afrika Kusini , Lunatic

Videio ya wimbo huo imefanywa nchini Afrika Kusini na Justin Campos.
Vanessa Mdee ameshinda mara kadhaa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award  na  All African Music Awards – AFRIMA kama Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki.
Posted by MROKI On Saturday, March 28, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo