Nafasi Ya Matangazo

March 30, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Machi 29, 2015 amewasili jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.
Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amefunguia rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, na Jumatatu Machi 30, 2015 amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
Rais Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya  Wawakilishi wa Kudumu kutoka nchi mbalimbali walioalikwa kushuhudia ufunguzi wa  jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akisalimiana na wakandarasi wa ujenzi  wa  jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiangalia picha za waliopata kuwa Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya  kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akiangalia picha za waliopata kuwa Wawakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya  kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Nyuma yake ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi
Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Joseph Msami wa Raido ya Umoja wa Matifa Idhaa ya Kiswahili kwenye ofisi hizo mara alipofungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Rais Kikwete akatika picha ya pamoja na baadhi ya Wa-Tanzania wanaoishi Marekani w baada ya kufungua  rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. PICHA ZAIDI FK MATUKIO
Posted by MROKI On Monday, March 30, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo