Nafasi Ya Matangazo

January 26, 2015

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza washiriki wa Mkutano huo umuhimu wa kuelimisha umma kuelekea upigaji kura ya maoni na kuwataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza suala hili la kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti Bw. Theophil Makunga akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pia aliwataka Maafisa Mawasiliano kutengeneza mazingira yatayowezesha kufanya kazi na wanahabari.
Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini leo Mjini Mtwara
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Bw. Innocent Mungy akiwasilisha Mada kwa washiriki wa Mkutano huo kuhusu wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya serikali kwa umma.
Mjumbe wa Jukwaa la wahariri Bw. Salim Salim akiwaeleza washiriki wa mkutano huo Umuhimu wa kuwa na Usiri katika utendaji kazi
Posted by MROKI On Monday, January 26, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo