Nafasi Ya Matangazo

October 28, 2014

Warembo wa Miss Universe Tanzania 2014  wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Golden Tulip  Hotel. Hii ni kwa ajili ya kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania 2014  itakayofanyika tarehe 02  mwezi Octoba.

Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti. 

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema usaili wa mwaka huu umefanyika katika mikoa mitano ya Tanzania na warembo zaidi ya 70 walisajiliwa kwa mashindano haya. 

Kambi ya Miss Universe Tanzania 2014 imekamilishwa na warembo 12 kutoka mikoa mitano ya Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam, pamoja na mrembo mmoja kutoka Zanzibar.

“Tumechagua warembo ambao wameonyesha uwezo wa kujitambua na kuelewa umuhimu wa kushiriki katika mashindano makubwa kama haya. Tuna wanafunzi wa vyuo wanaosomea udaktari, uhandisi,uhasibu na pia tuna akina dada wajasiriamali . Tunafurahi kuona kila mwaka warembo wetu wanazidi kujitambua na kazi yetu kubwa ni kuwaendeleza” alisema Sarungi

Pamoja na zawadi ya fedha taslimu, mshindi wa Miss  Universe Tanzania 2014 atapata fursa ya kutangaza bidhaa mbalimbali na kufanya kazi za kijamii. Pia kama ilivyo ada kwa mwaka wa 4 sasa, mshindi atapewa nafasi (scholarship) ya kusoma New York Film Academy , Marekani. Hivi sasa washindi wa mwaka 2011 na 2012, Nelly Kamwelu na Winfrida Dominique wako New York masomoni.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata James ,2010 Hellen Dausen  , 2011 Nelly Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaniwa na  Insignia, MeryLight , Golden Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Missie Popular blog, Seif Kabelele blog, Urban Rose Hotel, RichBoys Entertainment (TZ) Ltd  na New York Film Academy.
Posted by MROKI On Tuesday, October 28, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo