Nafasi Ya Matangazo

September 23, 2014



Na Fadhaer Kidevu Blog
BEKI mpya aliyesajiliwa na Yanga akitokea JKT Ruvu Edward Charls,huenda Jumapili akaanza kuichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya Oscar Joshua kusumbuliwa na nyama za paja.

Kocha mkuu wa Yanga Marcio Maximo,ameonekana akimwandaa beki huyo kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili wakati timu hiyo itakapokuwa uwanja wa taifa kuwakabili Prisons ya Mbeya.

“Niwazi sitoweza kumtumia Joshua kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya paja aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Mtibwa Jumamosi kwahiyo Charles anaweza kuziba nafasi hiyo kutokana na kufanya vizuri mazoezini,”anasema Maximo.

Huyo itakuwa mechi ya kwanza ya ushindani kwa Charles,aliyejiunga na Yanga mwishoni mwa siku za usajili akitokea kwa maafande hao wa JKT Ruvu.
Posted by MROKI On Tuesday, September 23, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo