Nafasi Ya Matangazo

September 01, 2014



Na Father Kidevu Blog
NAHODHA wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema haoni sababu ya viongozi na mashabiki wa timu hiyo kuhuzunika baada ya kuondoka kwa Emmanuel Okwi,kwani timu hiyo inawachezaji wazuri zaidi yake.

Ijumaa iliyopita klabu ya Simba ilitangaza kumsajili Okwi kwa mkataba wa miezi sita huku bado akiwa anamkataba wa miaka miwili wakuichezea timu hiyo ya Jangwani.

“Inashangaza kwa kitendo ambacho amekifanya mchezaji mwenyenzetu lakini viongozi wanapaswa kuachana naye kwa sababu anaonyesha Okwi anamapenzi na Simba lakini hata sisi tunakikosi imara ambacho kinaweza kufanya mambo makubwa bila yeye,”alisema Cannavaro.

Cannavaro ameiambia Father Kidevu Blog kuwa, mchezaji huyo hakuwa na umuhimu sana kwenye kikosi chao kama ilivyokuwa kwa Didier Kavumbagu au Frank Domayo waliotimkia Azam na hilo watalidhihirisha watakapokutana naye kwenye mechi ya Ligi Oktoba 12 mwaka huu.
Posted by MROKI On Monday, September 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo