Nafasi Ya Matangazo

September 01, 2014



Na Father Kidevu Blog
KOCHA Mkuu wa Simba Mzambia Patrick Phiri amesema kwa sasa kikosi chake kimekamilika na kipo tayari kwa mechi za Ligi Kuu.

Phiri ambaye aliiongoza Simba kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mabingwa wa Zanzibar KMKM juzi kwenye uwanja wa Amani,alisema haitaji kusajili mchezaji mwingine kwa sasa baada ya kuwasili kwa Emmanul Okwi.

“Hiki ndiyo kikosi cha ubingwa ambacho nilikuwa nakihitaji nafurahi nimekipata kwa muda mfupi tangu niliporudi Simba kwa sasa sihitaji kusajili mchezaji mwingine baada ya Okwi,”alisema Phiri.

Simba aliyopiga Kambi Visiwani Zanzibar imepania kufanya vizuri msimu huu baada ya kupita katika kipindi kigumu katika misimu miwili iliyopita na kupelekea timu hiyo kushindwa kumaliza hata nafasi ya pili.
Posted by MROKI On Monday, September 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo