Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2014



Na Magreth Kinabo,Dodoma
Mjumbe wa  Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe nchini , Mzee Kingunge Ngomabale Mwiru amesema  Katiba bora ni ile itakayozingatia  historia  mafanikio ya  miaka 50 iliyopita na Muungano imara.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mzee Kingunge wakati akichangia  katika mjadala wa Bunge hilo  juu ya uwasilishaji wa taarifa  za Kamati Namba Moja hadi Kamati Namba Kumi na Mbili za Bunge hilo kuhusu uhakiki wa Rasimu  ya Katiba  iliyopendekezwa.

Aidha Mzee Kingunge amesema  wameondosha mapendekezo ambayo yanataka kusambaratisha muungano ili uweze kuwa imara.  

Mzee Kingunge aliyataja mambo matatu ambayo yatazingatia Katiba  bora kuwa ni  ni ile itakayoimarisha historia ya mafanikio ya miaka 50 iliyopita, inayopunguza  na kuondoa kero mbalimbali za msingi.

Aliongeza  kuwa tatu ni “Lazima Katiba  Mpya iingize mambo  ambayo yataimarisha nafasi za wananchi mfano wakulima , wafugaji, wavuvi, wasanii na wachimbaji wadogo… Tanzania haitakuwa  kama ilivyokuwa huko nyuma baada ya mkutano huu.

“ Kwa sababu makundi yote yote yamekutana hapa kuzungumzia maslahi yao na hatma yao,” alisema Mzee Kingunge.

Mzee Kingunge alisema mawazo yaliyotolewa na ni ushindi mkubwa, kazi iliyobaki ni kupitisha.

“Kazi  hii si ndogo ni kubwa…kwani  kuna  zogo , lakini tumevulia napenda iandikwe kwa wino wa dhahabu kama ilivyo hapa ndani,” alisisitiza.   

Mwanasiasa huyo alifafanua  kuwa  Katiba ni maridhiano, hivyo anajua wakubwa wataendelea kuzungumza, hivyo katika hilo ni vizuri wakawa waangalifu.

“ Tuifanye kazi hii kwa unyenyekevu, wananchi  wanangoja Katiba bora,” alisema.
Posted by MROKI On Saturday, September 27, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo