Nafasi Ya Matangazo

September 01, 2014

 BRENDAN Rodgers jana alisherehekea kuiongoza Liverpool katika mechi ya 100 kwa ushindi  mwingine wa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Mario Balotelli alipoteza nafasi kadhaa akiwa amevaa jezi ya majogoo hao lakini pamoja na hayo haikuwa sababu ya Spurs kutopoteza mechi hiyo, na sasa imepata kipigo cha kwanza chini ya kocha mpya Mauricio Pochettino.

Liverpool, ambayo ilishinda mabao 5-0 msimu uliopita, jana iliongozwa na wafungaji wake Raheem Sterling aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya nane kabla mkongwe Steven Gerrard hajafunga  bao la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 49 na Alberto Moreno kufunga bao la tatu katika  dakika ya 60. 

Nayo Aston Villa ikiwa nyumbani iliichapa Hull City mabao 2-1 katika mechi nyingine ya Ligi Kuu  England jana.Mabao ya Villa yalifungwa na Gabby Agbonlahor katika dakika ya 14 na Andreas Weimann katika dakika ya 36. Hull ilipata bao lake katika dakika ya 74 likifungwa na Nikica Jelavic  baada ya kuuwahi mpira wa kichwa wa beki wa Villa Aly Cissokho. Villa ilimaliza ikiwa na  wachezaji 10 baada ya Ron Vlaar kutolewa nje kutokana na kuwa majeruhi.
Posted by MROKI On Monday, September 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo