Nafasi Ya Matangazo

September 17, 2014

Na Fadher Kidevu Blog
KIUNGO wa Brazili Andrey Coutinho,leo ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga kujiandaa na mechi ya kwanza ya Ligi itakayochezwa Jumamosi Morogoro dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar.

Coutinho,aliumia enka kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dar es Salaam na kulazimika kukoa mchezo wa Ngao ya Jamii Jumapili iliyopita ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 3-0,ambapo mawili yalifungwa na Mbrazili mwingine Geilson Santana Santos JAJA.

Daktari wa Yanga Juma Suphian,ameiambia Blog ya Fadher Kidevu Blog, kwamba mchezaji huyo ameanza mazoezi madogo na mwenzake Jeryson Tegete na watakuwemo kwenye safari ya Morogoro Alhamisi kwa ajili ya kuikabili Mtibwa Sugar.

Posted by MROKI On Wednesday, September 17, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo