Nafasi Ya Matangazo

July 28, 2014

 Sheikh Dlulkifilo Omari  kulia akiwa na baadhi ya  waumini mara baada ya  ibada hiyo  leo
  
Mmoja  kati ya  waumini  wa dini ya Kiislam waumini  wa madhehebu ya answaar Sunna iliyofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa akitoka kuswali  leo
********
Na Matukiodaima blog
Sheikh wa  msikiti  wa  Hidaya katika manispaa ya  Iringa  Dhulkifilo Omary  wa  amempongeza  Rais  Jakaya Kikwete  kwa jitihada zake  kubwa  za  kufanikisha Tanzania  kuanza mchakato wa  kupata katiba mpya na  kuwaonya wajumbe wa bunge la katiba  kurejea bungeni kuunda bora badala ya  kuendeleza mivutano isiyo na tija.

Akizungumza  leo  na  mtandao  huu  wa matukiodaimablog  mara  baada ya   swala ya  Idd  -el Fitr  kwa  waumini  wa madhehebu ya answaar Sunna iliyofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini  Iringa Sheikh  Omary  alisema  kuwa  kazi kubwa na nzuri  imefanywa na  Rais  Kikwete katika kuanzisha  mchakato wa katiba  ikiwa ni  pamoja na kuunda tume ya katiba na hadi  kufanikisha rasmu  hiyo ya katiba .

Hivyo  alisema  kuwa  wajibu  wa  wajumbe wa  bunge la katiba na kushiriki  kuandaa katiba ambayo italetwa kwa  wananchi kwa  lengo la  kuipigia kura  na  si  wakati wa  wajumbe hao  kuanza mivutano  isiyo kuwa na  tija  .


" Mimi  kwa  mawazo yangu  mimi kama sheikh  Omary  hawa  wajumbe  wa  bunge la katiba  walipaswa  kuketi  pamoja  bunge na  kutuletea katiba  nzuri na  sio  kutuletea  vurugu na malumbano  yasiyo kwisha  katika  bunge  hilo"

Alisema  kuwa vurugu  zinazoendelea  juu ya katiba   hiyo kwa  wajumbe  kuwa katika makundi makundi ni  wazi kuwa hakutakuwa na katiba mpya kwa  sana   iwapo makundi  hayo yataendelea
Posted by MROKI On Monday, July 28, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo